Jambo zuri pale ufanyapo biashara ni lands zote mbili kupata furaha baada ya kukamilika kwa biashara hiyo. Hivyo ndivyo inavyokuwa pale mteja anaponunua picha/mchoro toka dukani kwetu. Huwa tunahakikisha picha inawekwa vizuri ili ifike salama.
Hii hapo juu ni picha aliyotuma mmoja wa Wateja wetu baada ya kufika nyumbani kwake Russia na kuiweka ukutani. Hakuona sababu ya kutoonesha furaha yake.Na hapo juu ni rafiki zetu Mariana na Santiago Decia wakiwa na furaha baada ya kufika kwao Uruguay na kutuma picha inayoonesha mchoro walionunua walipotembelea Zanzibar mwaka 2016.
Karibu pia nawe ujipatie picha imara kwa ajili ya nyumbani kwako.
Comments
Post a Comment