Real Visual Media Production

Anaandika Peter Bulugu.

Laban P Msanzya ni jina lenye kusikika sana midomoni kwa watu wengi hapa Dodoma hasa pale linapokuja suala la kutafuta nani atafanikisha sherehe kwa upande wa video na picha mnato.



Ni kijana aliyeamua kukaa chini na kujifunza kazi kwa muda mrefu akiwa chini ya wakongwe katika tasniya hii hapa Dodoma. Hakukata tamaa akijua ipo siku ataanza kufanya kazi zake mwenyewe.


Wanasema hata mbuyu ulianza kama mchicha ingawa ni ngumu kuamini nadharia hii. Alianza na kamera moja kuukuu aliyonunua toka kwa mtu. Lakini sasa anamiliki studio yake ya kisasa inayofanya kazi nzuri za harusi, send-off, tafrija mbalimbali, kurekodi documentaries mbalimbali, kurekodi albamu za nyimbo, n.k



Wakati naandaa harusi Yangu sikupata tabu kujua ni nani atakayesimama katika kuhakikisha kumbukumbu za tukio hilo muhimu katika maisha ya binaadamu linachukuliwa katika ubora wa hali ya juu. 
Angalia kipande cha sehemu ya harusi Yangu hapa chini. 



Karibu uwasiliane nao katika anuani zilizopo hapo juu kwenye picha.
Tupambane kujiajiri vijana hata kama mwanzo unaonekana ni mgumu. Lakini ipo njia kwenye nia

Comments